Wizara ambazo bajeti zake zinaweza kuibua mijadala mizito
ni Wizara ya Elimu; Tamisemi; Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; Mambo ya Ndani; na Wizara ya Nishati na Madini.
Wizara
ya Elimu inatarajiwa kukumbwa na mjadala kutokana na kutochukua hatua
zozote tangu kuibuka kwa tuhuma za kughushi vyeti dhidi ya ofisa mmoja
mteule wa Rais.
Tangu tuhuma hizo zilipoibuka, si Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) wala Wizara ya Elimu iliyoibuka kuzungumzia suala hilo. Wizara hiyo inaendesha uhakiki wa vyeti vya elimu kwa watumishi wa umma.
Waziri
wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako, ambaye amekuwa akisisitiza uhakiki
huo, amekuwa kimya katika suala la vyeti vya ofisa huyo.
Mteule
huyo wa Rais aliingia katika sakata hilo baada ya kuwatuhumu na
kuwangaza wanasiasa, viongozi wa dini, wasanii na wafanyabiashara
kuhusika katika matumizi na biashara ya dawa za kulevya.
Tangu tuhuma hizo zitolewe dhidi yake, hajawahi kukiri wala kukanusha.
Mjadala mwingine unaotarajiwa kuibukia wizara hiyo ni sera ya utoaji wa elimu bure.
Hivi karibuni Taasisi ya Haki Elimu imetoa taarifa inayoonyesha changamoto za utoaji wa elimu bure ikionyesha mafanikio hafifu.
Mijadala
itakayoibuka katika Wizara ya Elimu inaweza kufanana na mijadala
itakayotokea Wizara ya Tamisemi inayosimamiwana George Simbachawene
inayosimamia wakuu wa mikoa na wilaya.
Hii
inatokana na wakuu hao kuwaweka ndani watendaji kwa makosa ya kinidhamu
kinyume cha Sheria ya Utumishi wa Umma inayoeleza bayana mamlaka za
kuchukua hatua dhidi ya watendaji.
Katika
mijadala iliyoibuka awali, mbunge wa Muheza, Adadi Rajab alishauri
wakuu wa mikoa na wilaya kuelimishwa kuhusu uchukuaji hatua na matumizi
ya Sheria ya Tawala za Mikoa na Wilaya.
Adadi
aliyewahi kuwa kamishna wa polisi na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa
ya Jinai (DCI), alisema suala la ukamataji ni taaluma inayosomewa.
Simbachawene pia ana kibarua cha kufafanua kuhusu changamoto za utoaji elimu bure.
Hali
kama hiyo inaweza kuibuka katika bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo ambayo kwa sasa inaongozwa na Dk Harrison Mwakyembe.
Suala
la waziri wa zamani, Nape Nnauye kutishiwa bastola na askari kanzu
wakati akienda kuzungumza na waandishi wa habari linaweza kuibua mjadala
wa uhuru wa habari na kujieleza.
Dk
Mwakyembe ana kibarua kigumu cha kufafanua kuhusu kukamatwa na kutekwa
kwa wanamuziki, na hasa Ibrahim Mussa maarufu kama Roma Mkatoliki.
Roma,
akiwa na wasanii wenzake, walitekwa na watu wasiojulikana wakiwa katika
studio ya Tongwe iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam na baada ya siku
mbili, walipatikana.
Habari za watu waliowateka na mazingira ya kuachiwa huru zimekuwa na utata na hakuna aliyeweka bayana hadi sasa.
Akichangia
katika mjadala wa hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu wiki iliyopita, mbunge
wa Chemba (CCM), Juma Nkamia alihoji sababu za Dk Mwakyembe kuhudhuria
ambao Roma alikuwa anazungumza na waandishi wa habari kuhusu kutekwa
kwake.
Hoja
ya Nkamia aliyewahi kuwa naibu waziri wa wizara hiyo katika awamu ya
nne, ilikuja huku baadhi ya wabunge wakiibana Serikali iwajibike kwa
matukio ya utekaji.
Hata hivyo, Dk Mwakyembe alijibu hoja hiyo ya Nkamia kuwa alikuwa Maelezo kwa kuwa ndiyo ofisini kwake.
Kabla
ya tukio hilo la Roma, Elibariki Emmanuel, maarufu kwa jina la Ney wa
Mitego, alikamatwa na Jeshi la Polisi baada ya kutoa wimbo wa “Wapo”
unaoelezea kuwepo kwa watu tofauti, akiwemo kiongozi mwenye vyeti vya
kughushi na kuhoji sababu za “mtumbua majibu” kutolitumbua “jipu jipya
mjini”.
Hata hivyo, Rais Magufuli aliagiza aachiliwe na auboreshe wimbo wake kwa kuongeza watu wenye sifa nyingine.
Katika muendelezo huo, matukio ya utekaji, ukamataji na mauaji dhidi ya viongozi wa vijiji, watendaji na askari wa Jeshi la Polisi, yanampa kibarua kigumu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba.
Katika muendelezo huo, matukio ya utekaji, ukamataji na mauaji dhidi ya viongozi wa vijiji, watendaji na askari wa Jeshi la Polisi, yanampa kibarua kigumu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba.
Mbunge
wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete alimtaka Waziri Mwigulu kutoendelea
kukalia kimya matukio ya utekaji, lakini siku chache baadaye polisi nane
waliuawa katika shambulizi la aina yake lililotokea Kibiti mkoani
Pwani.
Pia,
Waziri Mwigulu atakuwa na kazi nzito kutokana na kutotolea tamko
vitendo vya utangazaji na ukamataji wa raia vilivyofanywa na mteule wa
Rais kwa kuwalenga watu maarufu, wakiwamo wanasiasa, wafanyabiashara na
wasanii walitajwa.
Mbali
na masuala ya usalama, hatua ya Rais Magufuli kukamata makontena ya
mchanga wenye madini katika bandari ya Dar es Salaam, nalo linatarajiwa
kuzua mjadala bungeni.
Mbali
na kukamata mchanga huo, Rais Magufuli amemsimamisha kazi katibu mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justine Ntalikwa saa chache
baada ya kujibishana na ujumbe wa Spika Job Ndugai uliotembelea
bandarini kushuhudia makontena yenye mchanga wa shaba.
Suala
hilo lilishaanza kuibua mjadala kutokana na hatua ya kuzuia ghafla
mchanga huo, inayoonekana inaweka mazingira yasiyo rafiki kwa wawekezaji
ambao walishangia mikataba na Serikali kwa kutumia sheria za nchi.
Umoja wa wachimbaji wadogo uliiomba Serikali kuuachia mchanga huo kwa sababu unasafirishwa kwa kufuata utaratibu.
Tayari Rais Magufuli ameshaunda kamati mbili za wataalamu kuchunguza mchanga huo na kutoa mapendekezo.
Tangu mjadala wa mchanga huo uanze, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo hajatoa kauli yoyote
Post a Comment