DAR ES SALAAM: Ukaribu wa sexy lady wa Bongo Fleva, Hellen George ‘Ruby’
na MbongoFleva, Ali Salehe Kiba ‘King Kiba’, unadaiwa kuzua maswali kwa
kuwa, jamaa huyo siku chache zilizopita alimvisha pete ya uchumba
mwandani wake aitwaye Amina kutoka nchini Kenya.
Siku chache zilizopita uliibuka uvumi kuwa, mastaa hao kwa sasa wanatoka
kutokana na ukaribu wao ambao umezua gumzo huku swali la wengi likiwa
kama ni kweli hiyo ni ‘pea’ mpya Bongo, vipi kuhusu Amina?
Kufuatia ishu hiyo, Wikienda lilianza kwa kumtafuta Ruby na kumuuliza
kama taarifa za ‘kuchepuka’ na Kiba zina ukweli ambapo alijibu kwa
kifupi: “Sorry, sitaki kuulizwa kuhusiana na hayo mambo, naomba niulizwe
kuhusu kazi zangu tu!”
Post a Comment