Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
amewahimiza wananchi kudumisha na kuuenzi Muungano wa Taganyika na
Zanzibar na kuwahakikishia wananchi wa pande Mbili kuwa kero chache za
Muungano ambazo zimebaki zitamalizwa kwa mazungumzo kama hatua ya
kudumisha Muungano huo.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti
katika Mahojiano na vyombo Mbalimbali vya habari katika kuelekea katika
Kilele cha Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo
sherehe za kitaifa mwaka huu kwa mara ya Kwanza zitafanyika kwenye
Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Makamu
wa Rais amesisitiza kuwa tangu Muungano huo uasisiwe umekuwa na manufaa
makubwa kwa pande zote Mbili kwani jamii zimefahamiani na kushirikiano
vizuri katika shughuli za kiuchumi na za kimaendeleo hasa uimarishaji wa
ulinzi na usalama kwa wananchi wa pande Mbili.
Aidha,Amesema
hatua zinazochukuliwa za kutatua kero za Muungano kwa haraka ni jambo
jema na la msingi kwani linalenga kuhakikisha Muungano ambao umefikisha
miaka 53 sasa unakuwa ni Muungano wa mfano wa kuigwa Duniani.
Kuhusu
elimu ya Muungano wa Vijana, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan
amesema upo umuhimu mkubwa kwa taasisi za Kiserikali za pande Mbili
kuweka mikakati mizuri ya kuelemisha vijana wa sasa kujua umuhimu wa
Muungano ili waweze kuuelewa na kuudumisha.
Amesema
kwa sasa vijana wengi wanafuatilia sana mitandao ya kijamii hivyo ni
muhimu kwa taasisi za kiserikali zinazoshughulia Muungano kuweka
utaratibu wa kupeleka ujumbe mbalimbali kuhusu Muungano kwa jamii hasa
vijana kwa ajili ya kuwaelimisha faida za Muungano.
Makamu
wa Rais pia amehimiza makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo viongozi
wastaafu nchini waendelee na jitihada zao katika kuelimisha umma ili
kuuelewa vizuri Muungano kwa ajili ya faida ya jamii nzima na ya Taifa
kwa ujumla.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
DODOMA.
25-April-2017
Post a Comment