Wakuu salaam. Natumai tupo wazima. Kama inavyozunguka mitandaoni kuhusu
kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Mhe. John Heche, taarifa
hiyo ni ya kweli.
Mhe. Heche alifika Hospitali ya Taifa Muhimbili siku ya Jumanne wiki hii
kwa uchunguzi wa afya yake, baada ya uchunguzi wa awali alishauriana na
daktari wake na kukubaliana angerejea Hospitali baada ya wiki mbili kwa
matibabu rasmi.
Hata hivyo jana usiku Mhe. Heche alipata maumivu makali ya ghafla
tumboni na leo asubuhi alikimbizwa Hospitali Muhimbili na kufanyiwa
upasuaji (specialised surgery).
Upasuaji umeenda vizuri na hali yake inaendelea vema sana. Mwenyekiti wa Taifa Mhe. Freeman Mbowe amemtembelea kumjulia hali.
Salum Mwalim
Naibu Katibu Mkuu
CHADEMA
Jumapili April 16, 2017
Post a Comment