Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Bora Mhe. Angellah
Kairuki amebainisha baadhi ya mambo waliyokuwa wameyapa kiupambele
katika zoezi zima la uhakiki wa vyeti feki kwa kusema zoezi halikuweza
kuhusika na viongozi wa kisiasa.
Kairuki amebainisha hayo leo katika ukumbi wa Chimwaga uliopo ndani ya
Chuo Kikuu cha Dodoma, wakati anatoa taarifa ya uwasilishaji wa uhakiki
wa vyeti feki kwa Watumishi wa Umma lilioendeshwa na Serikali kuanzia
mwezi Oktoba mwaka 2016.
"Zoezi hili la uhakiki wa vyeti feki halikuwahusisha viongozi wa kisiasa
kama Wabunge, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, kwa sababu
kwa mamlaka za uteuzi wao wanahitajika kujua kusoma na kuandika
tu...Watumishi 9,932 wamebainika kuwa na vyeti vya kughushi sawa na
asilimia 2.4 . Wenye vyeti vya utata ni 1,538 vilikuwa vikitumiwa na
jumla ya watu 3,076, wenye vyeti halali pekee ni asilimia 94...Hatua
hazitachukuliwa kwa wenye vyeti feki tu, bali hata kwa wanaohusika
kutengeneza vyeti hivyo". Alisema Kairuki
Aidha Mhe. Kairuki amewataka wale wote wanajijua wanatumia vyeti vya
kughushi waache mara moja kwa kuwa ni kosa la jinai huku akisisitiza
kuwa adhabu yake ni kufungwa jela miaka saba.
Pamoja na hayo, Kairuki amepongeza serikali inayoongozwa na Rais Dkt.
John Magufuli kwa kuamua kushughulika na zoezi hilo na kulimaliza kwa
awamu moja tofauti na nchi nyingine zilichukua awamu tatu huku akitolea
mfano wa kwa kuzitaja nchi hizo kwamba ni South Africa na Nigeria.
Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Magufuli amewaagiza Waziri Kairuki na
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwaondoa watumishi wote waliobainika kuwa
wanatumia vyeti vya kughushi 'hewa' huku akisisitiza kwamba yeye hawezi
kuwasemehe watu walioghushi kwani wataondoka mara moja.
Post a Comment