Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewataka wanafunzi wa vyuo vikuu nchini na wananchi kutumia huduma za mawasiliano kwa faida, badala ya kuzitumia kujiburudisha pekee.
Mhandisi
wa Masafa wa TCRA, Francis Mihayo alisema hayo hivi karibuni wakati wa
kongamano la vyuo vikuu kujadili matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano (Tehama), lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Tumaini
Makumira mkoani Arusha. Mihayo alisema kumekuwa na matumizi yasiyo
sahihi ya mitandao hasa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambao baadhi
wameingia matatani kutokana na kuTOzingatia sheria.
Waziri
wa Habari na Mawasiliano wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho, John
Semindu alisema wameamua kuandaa kongamano hilo ili kutoa nafasi kwa
wanafunzi kujifunza matumizi sahihi ya na kujiepusha kusambaza ujumbe
wenye lengo la kusababisha uvunjifu wa sheria.
Semindu
alisema kutokana na kukua kwa huduma za mawasiliano nchini na duniani,
ni watu wachache wanaotumia huduma hizo zaidi ya kuwasiliana.
“Tunatakiwa
twende mbali zaidi ya kuwasiliana na kutumiana ujumbe kutufanya
tucheke, bali tunaweza kutumia huduma za Tehama kujiajiri na kuajiri
wengine ni eneo muhimu katika kurahisisha kazi na kuchochea ubunifu
ambao ndiyo msingi wa maendeleo,” alisema Semindu.
Richard
Gwele, kutoka Taasisi ya Smart Education na Mwangaza Jafar ambaye ni
mwanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, walisema elimu zaidi
inapaswa kutolewa ili kuepusha matumizi yasiyo sahihi hasa kwenye
mitandao ya jamii.
Gwele
alisema iwapo wanafunzi watatumia mitandao vizuri itawasaidia kupata
kujisomea mambo mbalimbali hasa yanayotokana na mabadiliko ya teknolojia
duniani.
Alisema wanafunzi hawajatumia hata nusu ya mitandao katika kujielimisha, hivyo wanatakiwa kubadilika.
Post a Comment