Na: Frank Shija – MAELEZO.
TPDC
kwa kushirikiana na Sekta binafsi wanatarjia kutekeleza miradi
mbalimbali ya usambazaji wa gesi asilian katika Mikoa ya Dar es Salaam,
Pwani, Lindi, Mtwara na baadhi ya mikoa mingine itakayoidhinishwa.
Hayo
yamebainishwa na Kiamu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya
Musomba wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake jana
Jijini Dar es Salaam.
Mhandisi
Musomba alisema kuwa miradi hiyo imeanza kwa kupitia upya taarifa ya
awali ya upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa mtandao wa bomba la
kusambazia gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo mnamo mwezi
machi 22, 2017 TPDC ilikaribisha jumla ya makampuni 9 ambayo yalikidhi
vigezo vya kimanunuzi kwa ajili ya kazi hiyo.
“Napenda
kuutaarifu umma kuwa TPDC inatarajia kutekeleza miradi mbaimbali ya
usambazaji wa gesi asilia katika mikoa ya Dar es Salaam, Bagamoyo na
Mkuranga Mkoani Pwani, Lindi na Mtwara pamoja na baadhi ya mikoa
mingine,” alisema Mhandisi Muyomba.
Aliongeza
kuwa lengo la kupitia upya taarifa za awali ni kuboresha zaidi taarifa
za kifedha, mahitaji ya kiufundi na utambuzi wa njia za kupitisha bomba
na ugawaji wa kanda za usambazaji.
Aidha
alisema kuwa ili kuharakisha usambazaji wa gesi, TPDC inakaribisha na
kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika uendelezaji wa miundombinu
itakayowezesha usambazaji wa gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam
mara tu mapitio ya upembuzi yakinifu utakapomalizika.
Mtandao
huo unakadiriwa kuwa na urefu wa takribani kilomita 65 ambao
utahudumia, kwa kuanzia, nyumba 30,000, viwanda na vituo vya kushindilia
gesi asilia pamoja na vituo vya kujazia gesi hiyo.
Katika
hatua nyingine Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema kuwa hadi sasa
TPDC imefanikiwa kukiunganisha na mtandao wa gesi asilia Kiwanda kimoja
cha kutengeneza Vigae cha Goodwill kilichopo Mkuranga, Mkoani Pwani huku
likiendelea na majadiliano na viwanda vingine vitatu kwa ajili ya
kuunganishwa na mtandao huo.
Kwa
mujibu wa Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015 TPDC inatambuliwa kuwa Shirika
rasmi la taifa linalojiendesha kibiashara, ambapo sheria hii inaipa
mamlaka TPDC kuruhusu makampuni mbalimbali kuendesha shughuli za sekta,
zitakazokuwa zainadhibitiwa kwa utaratibu maalum chini ya usimamizi wa
Mdhibiti anayetoa leseni.
Post a Comment