Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ameyasema hayo leo mjini Dodoma mara baada ya kukagua Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light) zilizofungwa uwanjani hapo.
Waziri Mbarawa, amesema kuwa hatua hiyo ni muendelezo wa uboreshaji wa uwanja huo katika kuruhusu ndege za aina zote kutua masaa 24 kwa wiki.
“Hii ni hatua ya pili ya uboreshaji wa uwanja huu ambapo hatua ya kwanza tumeimaliza ya upanuzi wa barabara za kuruka na kutua ndege (runway) hadi kufikia KM 2.5”, amesema Waziri Profesa Mbarawa.
Aliongeza kuwa ufungaji wa taa hizo umegawanywa kwa hatua tatu ambapo awamu ya kwanza imekamilika kwa kujumuisha ufungaji wa Mfumo wa Kisasa wa Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light), katika barabara za kuruka na kutua ndege na maeneo ya maegesho, hatua ya pili ni kufunga taa za kumsaidia Rubani kuweza kuona uwanja wote na hatua ya mwisho ni taa zitakazofungwa mita 400 kila upande uwanjani hapo.
Amefafanua kuwa taa hizo za kisasa (Aviation Solar Powered Light) zitapunguza gharama za uendeshaji uwanjani hapo ikiwamo matengenezo yake kwani zinadumu muda mrefu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara, Sekta ya Uchukuzi Dkt Leonard Chamuriho, amesema kuwa nia ya Serikali ni kuendelea kurefusha uwanja huo ambapo italipa fidia kwa nyumba zilizopo pembeni ya uwanja huo ili kuongeza usalama wa uwanja na ndege kwa ujumla.
“Tutaweka uzio katika uwanja huu kulingana na matakwa ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na pia kupitia uzio huu taa zitakuwa salama”, amesisitiza Dkt. Chamuriho.
Naye, Msimamizi wa mradi Samwel Mruma kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), amesema mfumo wa taa hizo za kisasa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light), zimefungwa kwa siku 14 na zina uwezo wa kufanya kazi kwa miaka 12 na kuwaka kwa masaa laki moja ukilinganisha na nyingine ambazo zinawaka kwa masaa elfu kumi.
Mfumo wa uwekaji Taa za Kisasa ni mkakati wa Serikali katika kuhakikisha inaendelea kuboresha viwanja vyake vya ndege ili kukidhi viwango vianavyostahili katika usafiri wa anga.
Post a Comment