Tangu uhuru wabunge wanakaa miaka mitano mitano na mambo yana enda iweje sahizi ndio ionekane haitoshi?? Je hii ya kutaka miaka saba ni la JUMA NKAMIA peke yake?? Au kuna watu nyuma yake? Jamani mnatuongoza wananchi si miti , NKAMIA imekuwaje Tena? Miaka mitano kuwa michache imeanza leo tangu 1985?
Jamani msicheze nakatiba yetu mtuachie nchi ikiwa salama tunawaomba sana acheni ubinafsi na tamaa ya madaraka toshokeni kama walivyo tosheka walio waruhusu na ninyi mkaipata nafasi hiyo, maana kila walio waachia hizo nafasi nao wangekuwa na tamaaa wakaongeza mda kama matakavyo kufanya ninyi hakika hata ninyi msinge zipata nafasi hizo.
Ukimya huu wa watanzani na upole wao msitake kuwatumia vibaya msifikiri hawajui kitu, tafadhari sana msicheze na katiba ya nchi msutulazishe kutuongoza bila hiyari yetu miaka mitano haitoshi??? Wakati wengine wana tawala miaka minne wewe mitano haikutoshi ?
Kwa masikio yangu nilimsikia Mh. Rais akisema kwa kinywa chake kuwa katiba sio kipaombele chake na ndio maana hata kwenye kampeni hakuongelea katiba hivyo naamini kuwa Mh. Rais hatokuwa sehemu ya mpango huu maana alikiri mwenyewe kuto hangaika na katiba , sasa nitashangaa kama kayageuka maneno yake mwenyewe, ndio maana huenda haya ni matakwa na NKAMIA na kundi lake kama hakuna aliye nyuma yake.
Post a Comment