0
Moto mkubwa ulitanda majira ya saa mbili kasoro za usiku mtaa wa usagara jijini Tanga ambao ulikuwa ukiteketeza nyumba ya makazi ya mtu binafsi chanzo kikiwa ni hitilafu ya umeme katika mfumo wa wiring wa ndani ya nyumba uliopelekea mlipuko wa moto mkubwa na wenye kasi ya hali ya ajabu kabisa, Licha ya ukubwa wa moto harakati za uokoaji zilizofanywa na Jeshi la zima moto la jijini Tanga kwa kushirikiana na zima moto kutoka mamlaka ya bandari Tanzania ( Tanga ) zilipelekea moto kuzimwa kabisa lakini hakuna mali yoyote iliyokolewa ndani ya nyumba hiyo.





Binmuswadick.com itakuletea habari kamili ikiwa ni pamoja na hasara nzima Jumla ya mali zilizoteketea ndani ya nyumba na mengineyo, Pindi itakapokuwa imefanikiwa kuwapata tena wahusika wakuu wa janga hilo.


HAKIKISHA UNAJIUNGA NASI KWENYE FACEBOOK TWITTER NA YOUTUBE ILI KUPATA BREAKING NEWS PINDI HABARI ZINAPOTOKEA

Post a Comment

 
Top