Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr.Reginald Mengi amewataka Watanzania kujitambua na kujiwekea malengo katika maisha ili kuepuka njia rahisi za kutafuta maisha ambazo baadhi zimekuwa zikiwagharimu baadhi ya wananchi hasa makundi ya vijana.
Akizungumza na wanafunzi wahitimu wa shule ya sekondari ya wasichana ya Kifungilo katika mahafali ya kidato cha nne kwenye taarifa yake iliyosomwa kwa niaba yake na Bi.Joyce Luhanga, Dr.Mengi amesema ukishajiwekea malengo ni rahisi kutafuta njia ya kuyafikia malengo hayo ili kukabiliana na changamoto za maisha zinazowakabili wananchi hasa makundi ya vijana.
Aidha katika taarifa ya Dr.mengi kwenye mahafali hayo yaliyohusisha na wageni kutoka mataifa mbalimbali,wazazi na viongozi wa serikali,dr.Mengi amewasisitiza wanafunzi wanaomaliza kuwa na mwenendo ulio bora kwa jamii kwa kufanya vyema katika mitihani yao ili waweze kufika vyuo vikuu.
Katika sherehe hiyo Mwenyekiti Mtendaji ameahidi shilingi 500,000 kwa kila mwanafunzi atakayepata alama (A) katika mitihani ya kitaifa inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni huku mkuu wa shule hiyo pamoja na mwakilishi wa wazazi wakielezea nafasi za wanafunzi wa shule hiyo katika mitihani yao ya mwaka jana hadi mwanzoni mwa mwaka huu.
Post a Comment