0
Baada ya Diamond kuvunja rekodi ya wimbo wake wa Hallelujah kwa kutazamwa zaidi na watazamaji wengi katika mtandao wa YouTube hatimaye ametolewa kileleni na msanii Aslay kwa video ya wimbo wake wa Natamba.
Hapo awali nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na msanii Diamond Platnumz na wimbo wake wa ‘Hallelujah’ wimbo ambao umekaa namba moja tangu ulipo achiwa Septemba 28, mwaka huu huku ukiwa na watazamaji zaidi ya million 3 mpaka sasa.
Wimbo wa natamba wa Aslay umepata mapokeo makubwa sana na kuzidi kuwadhihilishia mashabiki wake uwezo alionao hasa wa kutunga nyimbo kali ambazo amekuwa akizitoa mara kwa mara.
Aslay ni msanii pekee ambaye ametoa nyimbo nyingi zaidi kuliko wasanii wote kwa mwaka huu na wimbo wake huu ambao unatamba kwa sasa unatakribani ya watazamaji zaidi ya laki 4 mpaka sasa huku video hiyo ikiwa ina siku mbili tangu ilipowekwa kwenye mtandao wa YouTube.
Natamba imetayarishwa na Shirko huku video ya wimbo huo ikiongozwa na muongozaji mahiri kutoka hapa hapa nyumbani Hanscana.

Post a Comment

 
Top