0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameagiza hatua kali zichukuliwe dhidi ya Mkandarasi ambaye ametelekeza ujenzi wa mradi wa Umwagiliaji kwenye Gereza la Kilimo Idete mkoani Morogoro.
Agizo hilo limetolewa baada ya Naibu Waziri Masauni kutembelea gereza hilo kwaajili ya kujionea mradi huo ambapo alielezwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mzee Ramadhan Nyamka.
Baada ya Karani wa Ujenzi wa Mradi huo Mkaguzi wa Jeshi la Magereza, Juma Mtega, kumuonyesha Naibu Waziri Masauni, chanzo na hatua za ujenzi wa mradi hadi ulipotelekezwa mwaka 2016 ndipo Waziri akalitaka Jeshi la Magereza kufanya uchunguzi dhidi ya Mkandarasi huyo na ikithibitika anamakosa akamatwe na achukuliwe hatua za kisheria.
Mkandarasi huyo ametelekeza mradi huo wenye thamani ya shilingi Bilioni 2.5 tangu mwaka 2016 kitu ambacho kimemfanya Waziri Masauni atoe agizo hilo akisisitiza kumchunguza na kumchukulia hatua za kisheria endapo itathibitika Mkandarasi ana makosa.

Post a Comment

 
Top