Pondà ameachiwa leo Jumamosi jioni baada ya kushikiliwa na Jeshi hilo tangu jana Ijumaa asubuni akituhimiwa kutoa lugha za kichochezi katika mkutano wake na waandishi wa habari Jumatano iliyopita.
Msemaji wa Jumuiya hiyo, Sheikh Rajabu Katimba amesema: "Sheikh Ponda ameachiwa kwa dhamana na atatakiwa kuripoti tena polisi."
Awali, Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa alisema uchunguzi dhidi ya Ponda ulikuwa ukiendelea na kama ungekamilika angepewa dhamana.
"Upelelezi unaendelea na ukikamilika tutaangalia kama atapata dhamana au tutampeleka mahakamani," alisema Mambosasa kabla ya Sheikh Ponda kuachiwa.
Wakili wa Ponda, Profesa Abdallah Safari amesena: "Ni kweli Sheikh Pondà ameachiwa, ni lini atarudi tena sijajua ila sidhani kama watampeleka mahakamani."
Post a Comment