0

Image result for idris sultan
Mshindi wa Big Brother Africa 2014 Idris Sultan ameweka wazi vipimo vinavyoonyesha kuwa hana virusi vya ukimwi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Idris ameweka picha inayoonyesha karatasi yenye majibu ya vipimo ya afya yake alivyovifanya leo Ijumaa.

Karatasi hiyo inaonyesha kuwa hana virusi vya ukimwi wala homa ya ini.

Picha hiyo ilibebwa na ujumbe uliosomeka, "Barua ya wazi kwa  mwanamke ninayemtongoza ni matumaini yangu  hii itakufanya unipe moyo wako wote. Nimejaribu kufaulu lakini kama unavyoona vipimo vyote nimefeli na hakuna mtihani ninaoupenda kama kufeli.” 

Post a Comment

 
Top