Polisi Mkoa wa Arusha wameteketeza eka 17 za mashamba ya bangi katika Kata ya Kisimiri, wilayani Arumeru.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema mashamba hayo yalitekelezwa wakati wa msako maalumu.
Mkumbo
alitoa onyo kwa wananchi wanauzunguka Mlima Meru ambao wamekuwa
wakilima bangi kwa kisingizio kuwa, polisi hawawezi kufika.
“Kuna mtindo wa kulima bangi milimani hasa Mlima Meru, tunasema tutaendelea na msako kubaini wote wanaohusika,” alisema.
Aliwataka
viongozi wa mitaa na madiwani kuwa makini na kudhibiti kilimo hicho
haramu kwenye maeneo yao. Kamanda Mkumbo alisema kwa sasa umeanzishwa
mtindo wa baadhi ya wananchi kuchanganya bangi na mazao mengine ili
kupoteza ushahidi.
“Wanachokifanya
sasa wanachanganya miche ya mazao na bangi, kwa hiyo inakua pamoja
tutaendelea na msako huo kila kona lengo ni kuhakikisha kunakuwa na
ukomo wa kilimo hicho cha dawa za kulevya mkoani hapa,” alisema Mkumbo.
Post a Comment