Jumuiya ya Wanawake wa CUF (Juke- CUF) imewataka wanawake nchini kukataa kushirikishwa au kuwa sehemu ya utekelezaji wa mipango miovu dhidi ya chama hicho.
Mwenyekiti
wa Juke-CUF, Fatma Abdulhabib Ferej alisema hayo katika taarifa yake
kwa vyombo vya habari aliyoitoa mwishoni mwa wiki iliyopita ikimuunga
mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
Chama
hicho kipo kwenye mgogoro wa uongozi kati ya katibu mkuu huyo na
Mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa,
Profesa Ibrahim Lipumba.
Ferej
alisema si busara kwa mwanamke kujiingia katika kundi ambalo kwa
makusudi linaonekana kwenda kinyume na utaratibu wa sheria uliopo kuhusu
vyama vya siasa nchini.
Alisema
Juke-CUF ipo tayari kukilinda chama hicho kwa gharama yoyote na kwamba,
itasimamia na kutekeleza maagizo yatakayotolewa na CUF.
Ferej
alisema mgogoro huo umepandikizwa makusudi ili kufifisha mafanikio ya
CUF yaliyopatikana katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015.
Post a Comment