0
 
 
Wazee wanaoishi katika kambi ya makazi ya waathirika wa ukoma ya Misufini wilayani Muheza, wamemuomba Rais John Magufuli kuwaongezea mgawo wa chakula kwani wanachopata hakitoshelezi.
 
Walitoa ombi hilo juzi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanasha Tumbo wakati walipokabidhiwa mbuzi, mchele na mafuta ya chakula ikiwa ni zawadi iliyotolewa na Rais Magufuli kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka.
 
Mwenyekiti wa wakazi wa kambi hiyo, Bakari Salim alisema mgawo wa makopo mawili ya sembe ambayo wamekuwa wakipewa kila mmoja kila wiki hautoshelezi.
 
Akijibu maombi hayo, Tumbo aliahidi kuyafikisha kwa wahusika na kwamba ana imani yatapokelewa na kufanyiwa kazi.
 
Alitoa wito kwa wadau na taasisi nyingine kuunga mkono jitihada za Serikali za kuwalea wazee hao.

Post a Comment

 
Top