Korea Kaskazini imetoa onyo kwa maadui zake Jumamosi hii kwa kuonesha
silaha zake mpya na nzito kwenye gwaride la kijeshi mbele ya kiongozi
wake.
Pyongyang imeonesha silaha zake kadhaa kwa mara ya kwanza zikiwemo zile za kutumika chini ya maji.
Hiyo ni ishara kuwa inaweza kuishambulia Marekani au Ulaya bila shida.
Hatua hiyo imekuja katika kipindi ambacho Rais wa Marekani, Donald Trump
amekuwa akitweet kuwa kama China haiwezi kukabiliana na mpango wa
silaha za nyuklia wa Korea Kusini Marekani itainunua kesi.
Pia utawala wa nchi hiyo umeionya Marekani dhidi ya mashambulio yoyote inayopanga kufanya dhidi yake.
Gwaride hilo limefanyika kusherehekea miaka 105 ya kuzaliwa kwa babu yake Kim.
Kim anamshutumu Trump kulichokonoa taifa lake kijeshi kwa mfululizo wa
nyendo za kibabe ikiwemo kutuma meli kubwa ya USS Carl Vinson kwenye
peninsula ya Korea.
Post a Comment