Mwenyekiti
wa Kamati ya Uongozi, The Civic United Front (CUF) Julius Mtatiro
amefunguka na kusema chama cha CUF hakina walinzi wa chama wenye bastola
wala hakina walinzi wanaozunguka mitaani kufanya doria.
Julius
Mtatiro ametoa ufafanuzi huo leo baada ya Mkurugenzi wa Habari CUF
Taifa, ambaye anamuunga mkono Profes Ibrahim Lipumba ndugu Abdul
Kambaya kukiri kuwa ni kweli wao walituma vijana kwenda kwenye Kata ya
Mabibo kufanya doria.
"Siku
ambapo kikao kinafanyika Vinna Hotel, vijana wetu pia walikuwa kwenye
doria, tulipozungumza na vyombo vya habari tulikiri na tunaendelea
kukiri hatuna sababu ya kukataa kwamba tulituma vijana wetu na
walikwenda kwenye doria" alisema Kambaya
Kufuatia
taarifa hiyo ya Kambaya Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, The Civic
United Front (CUF) Julius Mtatiro amefunguka na kusema wao kama CUF
hawana walinzi wa chama wenye bastola hivyo amelitaka jeshi la polisi
limtumie huyu Kambaya kueleza kijana aliyekuwa na bastola yuko wapi na
walikodishwa kutoka wapi.
"Leo
amekiri kuwa lile Zombi lililopigwa na wananchi, Mabibo, eti lilitumwa
na genge la Mungiki/Lipumba ili kufanya doria kwenye kata ya Mabibo.
Yani eti Lipumba ana jeshi lake linalofanya doria na kupiga watu
mitaani. Sasa Polisi wasitafute mchawi, huyu Abdul Kambaya aeleze lile
zombi lililokuwa na bastola liko wapi na waliikodisha kutoka wapi?
Alihoji Mtatiro
Mbali na hilo Mtatiro alizidi kusisitiza kuwa wao hawana walinzi wa chama
"Halafu,
eti huyo msemaji wa Lipumba anasema "Zombi" hilo lililokamatwa ni
"mlinzi wa chama". Napenda ifahamike kuwa CUF haina walinzi wa chama
wenye bastola, na pia hakuna chama cha siasa chenye walinzi wanaozunguka
mitaani kufanya doria, wameajiriwa na serikali ipi? Alihoji Mtatiro
Post a Comment