Tende zimekuwa zikitumiwa na watu wengi hasa katika kipindi cha ramadhani, hata hivyo ukweli ni kwamba tende hazitakiwa kutumiwa katika kipindi cha mfungo pekee, bali inatakiwa kila wakati walau mara mbili kwa wiki mtu aweze kutumia tende.
Na zifuatazo ndizo faida za matumizi ya tende.
1. Ukila tende mara kwa mara, mwili wako utapata aina mbalimbali za madini na vitamin za kutosha, ambazo zinapatikana kwenye tunda hili maarufu duniani. Katika tende kuna kiasi kidogo tu cha mafuta (fat). Mafuta haya husaidia kutia joto na nguvu katila mwili wa binadamu.
2. Ulaji wa tende huimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji chakula tumboni, hivyo utaondokana na matatizo ya ukosefu wa choo, au matatizo ya kupata choo kigumu kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia. Pia ndani ya tende kuna virutubisho vya ‘amino acids’ ambavyo ni muhimu mwilini.
3. Ukila tende, mwili utapata nguvu na kukuondolea uchovu ndani ya nusu saa tu, kwa sababu tende ina virutubisho vya sukari asilia kama vile ‘glucose’, ‘sucrose’ na ‘fructose’. Ili kupata faida zaidi za tende,
changanya na maziwa fresh kisha kula. Unapojisikia mchovu, badala ya kunywa vinywaji baridi vinavyodai kuongeza nguvu, kula tende, hata kiasi cha punje tatu kinatosha. Kwa wafunga saumu, ndiyo maana inashauriwa kuanza kufungua kwa kula tende ili kuurejeshea mwili wako nguvu iliyopotea siku nzima.
4. Tende ina madini pia aina ya ‘potassium’ na kiasi kidogo cha chumvi (sodium). Madini haya husaidia uimarishaji wa mishipa ya fahamu. Watafiti wamegundua kwamba ulaji kiasi wa ‘potassium’ huweza kumuepusha mtu na kupatwa na kiharusi (stroke). Pia tende husaidia kupunguza lehemu (cholesterol) mwilini (LDL Cholesterol).
5. Kwa wale wenye matatizo ya ugonjwa wa kukauka damu mwilini (anemia), wanaweza kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi ambayo ina kiwango cha kutosha cha madini ya chuma ambayo huhitajika katika utengenezaji wa damu mwilini. Wakati vitu vitamu vingine huozesha meno, utamu wa tende huzuia uozaji wa meno.
Hizo ni baadhi ya faida chache kati nyingi zinazomsaidia mtu katika kutibu na kuzuia magonjwa mbalimbali.
Post a Comment