Ni siku chache tu zimepita tangu msanii Harmorapa atueleze juu ya ugeni alioupata wa msanii Kriticos kutoka Belgium ambaye amekuja Tanzania kufanya naye collabo akisema kuwa collabo hiyo haitachukua muda mrefu mpaka kukamilika.
April 14, 2017 Harmorapa aliialika waandishi wa habari kushuhudia maandalizi ya wimbo huo aliomshirikisha Kriticos ambao unatayarishwa kwenye studio za Bongo Records chini ya producer mkongwe P Funk ‘Majani’.
“Kriticos alikuwa anaimba kwa Kiingereza, sasa mimi mwenyewe Kiingereza cha kuungaunga, kuna saa nampata halafu simpati. Nikamuomba mkubwa mwenyewe Majani anisaidie kidogo kwa sababu mwenzangu yai linatema.” – Harmorapa.
“Tulikuwa studio na P Funk alikuwa anatusikilizisha baadhi ya beats, ndio akatusikilizisha hiyo moja ambayo ametengeneza kutumia simu yake. Tulivyoisikiliza tukawa tumeielewa. Mimi na Ronei (msanii mpya aliyekuwepo studio wakati huo) tukapata mizuka tukatengeneza wimbo; tukaingiza mistari. Yeye alifanya chorus ikabaki sehemu ya Harmorapa.” – Kriticos.
Post a Comment