Kuna wakati mwingine watu hushindwa kulitekeleza jambo fulani sio kwa sababu hawajui jambo hilo au eti kwa sababu hawana uzoefu wa jambo hilo, la hasha huo si kweli watu wengi wanashindwa katika kulifanya jambo fulani kwa sababu wanakosa"umakini" juu ya kulitenda jambo hilo.
Na umakini ni ile hali ambayo ambayo mtu anakuwa nayo kutoka nafsini mwake katika kulitenda jambo fulani, lakini kulitenda jambo hilo bila kufikiri ni sawa na bure, hivyo kila wakati unahitaji kujenga umakini kwa kuwekeza nguvu na akili katika kufikiri na kutenda jambo hilo.
Kamwe hutoweza kufanikiwa kama utaendelea ile tabia ya kutofanya vitu kwa umaikini. Kwani siri kubwa ya kushindwa kufanikiwa kwako ipo katika jambo hilo. Nasisitiza swala hili la kutenda mambo kwa umakini kwani pindi mtu anaamua kuwa makini humsaidia mtu huyo kuongeza ufanisi wa kiutendaji wa jambo husika na mara nyingine kutenda jambo kwa umakini huumfanya mtendaji wa jambo hilo kuepuka kurudia makosa katika kulitenda jambo hilo.
Hivyo umakini katika kila nyanya na masuala mbalimbali ya maendeleo yako binafsi na ya jamii kwa ujumla yanahitajika kwa kiasi kikubwa, hivyo kama unataka kufanikiwa kwa kiwango kikubwa unatakiwa kuwa makini kwa kila jambo.
Mwisho jitahidi kuwa makini juu ya mambo haya;
1. Kuwa makini katika kuchagua mawazo ya mambo ambayo unataka kuyatenda.
2. Kuwa makini katika kubeba mawazo na ushauri wa watu mbalimbali ambao wanakuzunguka. Au kwa maneno mengine tunaeza kusema kuwa makini na wewe mwenyewe na watu wengine.
3. Jitahidi kadri uwezavyo kuwa makini katika katika kufanya upembuzi yakinifu ni wapi ambapo umetoka ni wapi ambao unaelekea.
4. Kuwa makini katika katika kuchagua marafiki wenye tija kwako kila wakati.
5. Kuwa makini katika kuwekeza mambo ambayo unajifunza mara kwa mara. Jiulize yana tija gani kwako.
6. Kuwa makini katika kutambua thamani ya muda na pesa.
Hayo ni baadhi ya maeneo machache kati ya mengi ambayo unatakiwa kuwekeza fikra katika kulitenda jambo fulani.
Post a Comment