0
Image result for serie a & kim jong un 
Roma, Italia. Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-UN amejibainisha kuwa ni shabiki mkubwa wa Ligi Kuu Italia ‘Serie A’.
Hayo yalibainika muda mfupi baada ya kinda wa miaka 18 Kwang-Song Han kufunga bao kwenye klabu yake ya Cagliari nchini Italia hivi karibuni.

Seneta wa Italia, Antonio Razzi hivi karibuni alipokutana na wawakilishi wa nchi za bara Asia, alielezwa kwamba siyo tu Rais Kim amekuwa akifuatilia maendeleo ya mshambuliajia Kwang-Son, pia ni shabiki mkubwa wa ligi hiyo kwa ujumla.

Rais huyo wa Korea yeye ni shabiki mkubwa wa timu za Italia na mara kwa mara hufuatilia mechi za timu hizo zinapocheza.

Kiongozi huyo anayeonekana kama dikteta, ilielezwa kwamba amekuwa akifuatilia kwa karibu ligi ya Seria A na maendeleo ya mchezaji wa nchi yake, Kwang-Son.

Pia amekuwa mchezaji wa kwanza kutoka bara hilo kufunga bao kwenye Ligi ya Seria A.

Klabu ya Cagliari ilimsajili mchezaji huyo tangu Februari mwaka huu na mkataba wake utamalizika 2022.

Mchezaji mwingine wa Korea Kaskazini alisajiliwa klabu ya Fiorentina mwaka jana na amekuwa akicheza kwenye timu ya vijana kabla ya kutemwa mwishoni mwa mwaka 2016. 

Post a Comment

 
Top