Man Fongo amebainisha hayo katika kipindi cha eNewz huku akiendelea kuweka bayana baadhi ya mambo kuwa alitaka kudhulumiwa kufanya tangazo bila ya kupewa pesa stahiki.
“Mesen alianiambia nimpe kitambulisho changu mimi nikampa bila ya kumuuliza chochote kwa kuwa nilijua anataka kunipa msaada wa kunitangaza katika kazi zangu ili nipate riziki. Kumbe yeye lengo lake lilikuwa ni kwenda kuchukua pesa kwenye mtandao wa simu kama milioni 15 au 10 ili awafanyie tangazo bila ya mimi kujua. Baada ya hapo akanipigia simu ya kunitaka Jumapili niende studio na kunilazimisha nitengeze tangazo halafu anipe laki 2”. Alisema Man Fongo
Vilevile msanii huyo amesema alikataa kufanya tangazo hilo kwa kuwa aliona halina mashiko kwa malipo anayotaka kulipwa.
Kwa upande mwingine Man Fongo amesema hana ugomvi na aliyekuwa msimamizi wa kazi zake hapo awali Gmaker kama watu wanavyomzushia.
Post a Comment