0

Kiongozi wa Umoja wa Afrika Alpha Conde ambaye pia ni rais wa Guinea amezitaka nchi za Afrika zikate mahusiano yake na Ufaransa.
Akizungumza katika mkutano mjini Meknes nchini Morocco rais Alpha amesema anaamini kuwa endapo nchi za Afrika zitakata mahusiano yake na Ufaransa basi itakuwa mwanzo wa maendeleo.

Vilevile rais huyo amesema kuwa wakati umefika kwa nchi za Afrika kujisimamia na kutoruhusu nchi za  Ulaya kuingilia kila suala.

Aidha ametaka nchi za Afrika ziweze kuwa na demokrasia kama zinavyotaka zenyewe na si zitakavyo nchi za nje.

Toka awe mwenyekiti wa AU mwezi Januari,Conde amezitaka nchi za Afrika zisiburuzwe na nchi za nje.

Kwa mujibu wa habari,Conde alitamka matamshi ya kuachana na Ufaransa toka mkutano uliopita Abidjan.

Post a Comment

 
Top