Msanii wa bongo fleva, Juma Jux mwenye 'hit song' ya 'Unanikamata'
amefunguka mazito na kusema yeye na mpenzi wake Vanessa Mdee wapo sawa
kabisa hawana ugomvi ila wamemua kufanya hivyo kutokana na madai ya watu
kusahau kazi zao za muziki.
Jux amefunguka hayo baada ya kuwepo zile tetesi za muda mrefu katika
mitandao kijamii kwa kile kinachodaiwa wawili hao kutokuwa na maelewano
mazuri kwa sababu ya kuonekana Vanessa Mdee akiwa na mwanaume mwingine
anayedaiwa kuwa ndiyo mpenzi wake mpya.
"Mimi na Vanessa tupo sawa kabisa, tumeficha uhusiano kwa sababu
watu walianza kusahau hadi kazi zetu. Siwezi kuchukia kumuona Vanessa
akipiga picha na wanaume kwa sababu ile ni kazi yake, mimi nikikaa na
wasichana 10 watu watasema Jux ana-shoot lakini Vee akipiga picha na
wanaume 15 utasikia 'malaya' yule....Wasichana kwenye 'Industry' wako
wachache inabidi tuwasapoti....siwezi ku-mind kisa kapiga picha na Ice
Prince". Alisema Jux
Post a Comment