Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka 2013 ya shirika la OECD ambayo 27/7
Wallstreet waliinukuu, hizi ndizo nchi kumi zinazoongoza kuwa na wasomi
duniani. Tunapozungumzia wasomi, ni ile idadi ya watu waliomaliza elimu
ya vyuo vikuu na walau mtu kua ana digrii moja.
Namba 1:
Russian Federation.
Nchi hii inayoongozwa na Rais Vladimir Putin ina jumla ya watu Milioni
144.1 (2015) kwa mujibu wa Banki ya dunia na ina jumla ya kiwango cha
elimu ya chuo kwa asilimia 53.5.
Namba 2:
Canada.
Nchi hii iliyopo Kaskazini Amerika yenye jumla ya watu 35.85 million kwa
sensa ya mwaka (2015 ) Kutoka Benki ya dunia , Canada ina kiwango cha
elimu ya chuo kwa 51.3%.
Namba 3:
Japan.
Kwa mujibu wa Benki ya dunia kwa mwaka 2015, Japan ina watu wapatao
milioni 127, na ni nchi inayoongoza kwa Teknolojia na Sayansi duniani.
Japan ina kiwango cha elimu ya chuo kwa 46.4%.
Namba 4:
Israel
Nchi ya Israel ina kiwango cha elimu ya chuo kwa jumla ya 46.4%.
Namba 5:
United States
Nchi hii iliyopo katika bara a Amerika ipo katika nafasi ya tano ikiwa na kiwango cha elimu ya chuo 42.5%.
Namba 6:
Korea
Sensa ya mwaka 2015 chini ya Benki ya dunia ilibainisha uwepo wa watu
wapatao milioni 50.62 nchini Korea, ikiwa ina kiwango cha elimu ya chuo
40.4%.
Namba 7:
United Kingdom
Ikiwa ipo chini ya utawala wa Malkia Elizabeth wa pili na Waziri Mkuu
Theresa May, Nchi hii yenye wakazi wapatao milioni 65.14 ina kiwango cha
elimu ya chuo 39.4%.
Namba 8:
New Zealand
Nchi hii iliyopo kusini mashariki mwa Bahari ya Pacific,imeshika nafasi
ya nane ikiwa na wakazi wapatao milioni 4.596. New Zealnd ina kiwango
cha elimu ya chuo 39.3%.
Namba 9:
Finland
Nchi hii inapatikana Kaskazini mwa Bara la Ulaya, huku lugha zake zikiwa
ki Finishh na Kisweden. Taifa hili lina kiwango cha elimu ya chuo
39.3%.
Namba 10:
Australia
Ikiwa imezungukwa na Bahari ya Hindi pamoja na Pacific, Australia ina
wakazi wapatao miloni 23.75 kwa mujibu wa Benki ya Dunia mwaka 2015.
Kiwango cha elimu ya chuo ni asilimia 38.3.
Post a Comment