Dar es salaam: Huku tukio la msanii wa Hip Hop, Ibrahim Mussa ‘Roma
Mkatoliki’ na wasanii wenzake watatu kutekwa studio likiwa bado
halijapoa, mwinjilisti aliyefahamika kwa jina la Onoratus Mwinuka (51),
mkazi wa Mabwepande jijini Dar, amedaiwa kutekwa na kuuawa kisha mwili
wake kufukiwa ardhini huko Mabwepande, Risasi Jumamosi linakudadavulia.
HABARI KAMILI Kwa mujibu wa dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina
la Veronica Mwinuka, taarifa za kupotea kwa kaka yeka alizipata Machi
14, mwaka huu kutoka kwa watoto wa marehemu ambapo walisema tangu baba
yao alipoondoka alfajiri ya Machi 13, mwaka huu hakuwa amerejea tena
nyumbani.
Veronica aliendelea kusema watoto hao walimwambia pia katika alfajiri
hiyo ya saa kumi, marehemu aliondoka na mfanyakazi wake wa kiume aitwaye
Ayubu aliyekuwa na kawaida ya kumsindikiza kila mara kutafuta usafi ri
ili apeleke maziwa ya ng’ombe mjini kisha akishapata usafi ri yeye hurudi
nyumbani.
Inadaiwa kuwa, siku hiyo, walipofi ka kituoni, lilitokea gari aina ya
Toyota Noah, wakamuuliza marehemu kama anakwenda, akakubali na kupanda,
gari likaondoka.
“Baada ya hao watoto kunipa taarifa hizo sikuweza kushituka mara moja
maana nilifahamu pengine kaka alikuwa amepitia kwenye shughuli zake
nyingine za kiuinjilisti maana alikuwa ni muinjilisti lakini baada ya
kupita siku hiyo aliyopotea, siku iliyofuata kuna wizi ulitokea nyumbani
kwake ndipo nikashituka,” alisimulia Veronica.
WIZI WATOKEA NYUMBANI KWA MAREHEMU
Veronica aliendelea kusema kuwa, wizi huo uliofanyika ulifanywa na mmoja
wa wafanyakazi wa marehemu ambaye aliiba fedha zinazokadiriwa kufi ka
shilingi milioni 30 ambazo marehemu alikuwa amezitoa benki siku moja
kabla ya kupotea kwake kwa ajili ya kununua gari ndogo (pick up) ya
mizigo na kuwalipia wanaye ada ya shule.
“Kiukweli niliona si hali ya kawaida hasa nilipounganisha matukio ya kuibiwa nyumbani na kupotea kwake.
“Lakini mbaya zaidi kaka nyumbani alikuwa amebaki mwenyewe. Mkewe
alikuwa nyumbani kwao kwa ajili ya kumuuguza mdogo wake, kwa hiyo
niliamua kuwataarifu ndugu zangu wengine, akiwemo shangazi yetu ambapo
akatutaka tutoe taarifa kwenye vyombo vya usalama.”
ATAFUTWA MPAKA MOCHWARI
“Mkewe pia alirudi, tukaenda kwenye ofisi za serikali ya mtaa kisha
kwenye Kituo cha Polisi Mabwepande ambako tulitoa taarifa na kupewa RB
ili kumtafuta yeye pamoja na mfanyakazi yule aliyeiba.
Kazi ya kumtafuta sehemu mbalimbali ikaanza ikiwemo mahospitalini,
mochwari na sehemu nyingine mbalimbali lakini hatukuweza kumpata kaka
kwa zaidi ya siku ishirini baadaye,” alisema Veronica.
AZIDI KUSIMIULIA
Dada huyo wa marehemu aliendelea kusema kuwa, ilifi ka hatua ndugu
wakakata tamaa kwamba hawezi kupatikana tena, lakini hivi karibuni mdogo
wao mwingine wa mwisho aitwaye Alphonsia Mwinuka alifi ka kutoka Mbozi,
Mbeya kwa ajili ya kazi hiyo ya kumtafuta kaka yao.
Baada ya kufi ka akishirikiana na kijana wa kazi (Ayubu) aliyekuwa na
marehemu siku ya mwisho kuonekana pamoja na watoto wa marehemu, walianza
msako upya katika misitu inayozunguka nyumba ya marehemu.
SIKU YA MWILI KUONEKANA
“Kiukweli siku hiyo tulimtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio. Giza
lilipoanza kuingia mimi nilikuwa tayari nimechoka, nikamwambia Ayubu
pamoja na mtoto wa marehemu aitwaye Daniel mwenye miaka kama saba
kwamba, waende upande mwingine kumtafuta mimi nikarudi nyumbani.”
DALILI ZA KUONEKANA MWILI WA MAREHEMU
“Baada ya muda walirudi na kuniambia kuna sehemu porini ilichimbwa, pia
ilikuwa na ufa jambo lililoashiria kwamba kuna kitu kilizikwa.
Ayubu alisema alipatilia shaka hivyo kupapiga picha kwa kutumia simu
yake ya kisasa (smart phone). “Baada ya kunionesha na mimi zile picha
niliitilia shaka ile sehemu.
Lakini sikuongea jambo lolote mpaka siku iliyofuata, tulitoa taarifa
kwenye vyombo vya usalama na kwenda kwenye eneo lile tukiambatana na
wananchi wa mtaa ule, lengo ni kuangalia pale mahali palizikwa nini,”
alisema Alphonsia.
ENEO LA TUKIO
Alphonsia alisema, walipofi ka jirani na eneo hilo aliloliona kwenye
picha mnato za simu, cha kushangaza, yule kijana akaanza kuwazungusha,
lakini baada ya kumbana aliweza kuwaonesha na baada ya kuchimba
waliukuta mwili wa marehemu ukiwa umeharibika sana.
“Kiukweli ilitusikitisha mnomno, hatukuweza kuamini kuwa mwili tuliokuwa
tunauona ulikuwa ni wa ndugu yetu, hasa baada ya mkewe kuyatambua
mavazi. Kutokana na tukio lenyewe ilionesha ndugu yetu alitekwa na watu
waliomuua kisha wakamzika pale.
“Ni vigumu kufahamu sababu hasa ilikuwa nini lakini ni jambo lililoibua
maswali mengi yasiyokuwa na majibu. “Baadaye polisi walipokuja,
walimchukua Ayubu kwa ajili ya kwenda kusaidia upelelezi na mwili wa
marehemu ulipelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya
taratibu zingine za kipolisi,” alisema Alphonsia.
TAMKO LA SERIKALI YA MTAA
Naye mwenyekiti wa mtaa huo, Abdallah Omar alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo ambapo alilaani vikali matukio ya utekaji nyara yanayoendelea
nchini na kusema ni kinyume na haki za binadamu. Mwili wa marehemu
ulizikwa juzi Alhamisi kwenye Makaburi ya Mabwepande. Ameacha mke na
watoto wanne.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Matukio ya utekaji yanazidi kushamiri nchini, hadi sasa rekodi
inaonesha, waliowahi kutekwa ni Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ben Saanane (hajapatikana), aliyekuwa
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media, Absolom Kibanda
(alijeruhiwa), Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari, Dk. Steven Ulimboka
(alijeruhiwa) na Roma Mkatoliki (alijeruhiwa) na wenzake watatu.
Hata hivyo, baadhi ya matukio hayo yamekuwa yakihusishwa kufanywa na
wabaya wa waathirika hao ambapo baadhi ya wabunge, akiwemo Mbunge wa
Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, hivi karibuni alitoa hoja ya
kuundwa kwa kamati teule ya bunge kuchunguzaa matukio hayo.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, kwa upande wake alisema
serikali inachunguza matukio hayo ili kuwabaini wanaofanya vitendo
hivyo.
Post a Comment