0

Geoffrey Kirui aliongeza kasi ikiwa imesalia maili nne katika mbio za Boston Marathon hatua iliomfanya kufanikiwa na kushinda mbio hizo upande wa wanaume kwa muda wa saa 2 dakika 9 na sekunde 36.
Raia wa Marekani Galen Rupp alimaliza wa pili sekunde 21 nyuma ya Kirui.
Ni ushindi wa kwanza wa Kirui, Alimaliza wa saba katika mbio za marathon za mwaka jana mjini Amsterdam na watatu katika mbio za Rotterdam.

Wakati huohuo Edna Kiplagat alitimka mbio akiwa miongoni mwa kundi la wanariadha waliokuwa mbele na kukosa mpinzani kabla ya kushinda mbio hizo upande wa wanawake.

Kiplagat alimaliza katika muda wa saa 2 dakika 21 na sekunde 53 ikiwa na mara yake ya kwanza kushiriki mbio hizo.

Afisa huyo wa polisi kutoka Kenya mwenye umri wa miaka 38 aliwahi kushinda mbio hizo mjini London na New York.

Rose Chelimo pia wa Kenya aliyechukua uraia wa taifa la Bahrain alimaliza wa pili huku Mmarekani Jordan Hasay akiwa wa tatu.

Bingwa mtetezi wa mbio hizo kutoka Ethiopia Atsede Baysa wa Ethiopia hakuweza kumaliza miongoni mwa wanariadha 10 bora.

Post a Comment

 
Top