Rapa Nay wa Mitego amewapa neno baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kubeza tukio la kutekwa na kuteswa kwa Roma Mkatoliki, akieleza kile anachokiamini.
Nay amefunguka saa chache baada ya kuweka posti inayoonesha kuwa kuna watu wanafanya maigizo, hali iliyopelekea baadhi ya watu kuihusisha na tukio la Roma.
Akifunguka kupitia East Africa Radio jana, Nay alidai kuwa watu wanaodhani Roma alikuwa anafanya maigizo wanatenda dhambi kwani yeye anachokiamini tangu alipomuona hadi alipotoka hospitali ni kwamba tukio hilo ni la kweli na linaumiza.
“Mimi sikumlenga mtu yoyote, kwa watu ambao wamepeleka kwa upande wa Roma inabidi niwalaumu sana. Kwa sababu mimi ninachoamini tangu siku ya kwanza ambayo tumepata taarifa Roma amepata matatizo mimi sikupata usingizi. Mpaka nilipopata taarifa ndugu yetu amepatikana na yuko Osterbay Polisi,” alisema Nay.
“Na nilikaa mpaka mwisho, mpaka tunakaa tunaenda hospitali na tunazungumza. Sikumlenga Roma, ni dhambi pia. Kwa sababu mimi ninaamini alipata matatizo. Mimi hicho ndicho ninachoamini na sitaki kujenga picha nyingine,” aliongeza.
Roma alipotea kwa takribani siku tatu na baada ya kupatikana alisimulia mkasa wa kutekwa na watu wenye silaha akiwa na wenzake watatu katika studio za Tongwe Records, kisha kupelekwa kusikojulikana na kuteswa huku wakihojiwa kabla ya kutelekezwa kwenye ufukwe wa bahari katika eneo la Ununio jijini Dar es Salaam.
Hivi karibuni, mke wa Roma aliweka kwenye mtandao picha ya mumewe akiwa anaugulia maumivu nyumbani huku akiwa karibu na mwanae Ivan.
Post a Comment