Ameyasema hayo mapema hii leo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa Tanzania iko tayari kupeleka madaktari endapo Kenya itakuwa na uhitaji wa madaktari kutoka nchini kwani kuajiriwa kwa madaktari waliokuwa tayari kwenda kufanya kazi nchini humo hakuja vuruga uhusiano wowote.
“Tanzania tuna madaktari wengi sana ambao bado hatuna uwezo wa kuwa ajiri wote kwa wakati mmoja Serikalini au kwenye Sekta binafsi, kwa hiyo kama wakimaliza mgogoro wao walionao na mahakama sisi tuko tayari,”amesema Ummy.
Hata hivyo, Ummy ameongeza kuwa Tanzania inadharisha madaktari takribani 1200 kwa mwaka hivyo kama Kenya watahitaji watakuwa wamesaidia katika kutatua tatizo la ajira nchini.
Post a Comment