Rais wa Marekani
Donald Trump amekuwa akizungumza kuhusu maisha ya awali kabla ya kuwa
rais na kueleza jinsi wajibu wake huo mpya katika Ikulu ya White House
ni ngumu.
Trump alisema aliyapenda maisha yake ya zamani kwa
sababu ni mengi yalikuwa yakifanyika, alipozungumza na shirika la habari
la Reuters akiwa White House."Hii ni kazi nyingi zaidi kuliko ya maisha yangu ya awali, alisema. "Nilifikiri itakuwa rahisi."
Matamshi yake Trump ya kuwa rais yamejadiliwa katika mitandao ya kijamii, wengi wakielezea mshangao wao.
"Ninakosa maisha yangu ya awali," alisema Trump.
Post a Comment