Bunge nchini Ujerumani limepiga kura ya
kuunga mkono wafanyikazi wa serikali kutovaa vazi la kiislamu
linaloficha uso la Niqab wakati wanapokuwa kazini.
Mswada huo sasa utapelekwa katika bunge
kuu ili kuidhinishwa. Waziri wa maswala ya ndani Thomas de Maiziere
alisema kuwa hatua hiyo imeweka wazi viwango vya uvumilivu miongoni
jamii nyengine nchini humo.
Mnamo mwezi Disemba ,chansela wa
Ujerumani Angela Merkel alitoa wito wa kupigwa marufuku kwa vazi hilo
linalofunika uso linalovaliwa na wanawake kadhaa wa Kiislamu.
Vyama vya mrengo wa kulia vimekuwa vikishinikiza kupigwa marufuku katika maeneo ya ummakama vile nchini Ufaransa.
Zaidi ya wahamiaji milioni moja ,wengi
wao wakiwa waislamui kutoka mashariki ya kati wamewasili nchini
Ujerumani katika kipindi cha miaka miwili iliopita.
Post a Comment