0
Suala la manyayaso dhidi ya wahamiaji yamekuwa yakipigiwa kelele ulimwenguni kote na sasa hata roboti ya kwanza imekuwa ikitoa ushauri wa kisheria kwa wahamiaji jambo ambalo limeonekana limeleta afuheni kwa wahitaji.

Teknolojia ya kutumia roboti imekuwa ikishika kasi kwani roboti anaweza akamfanyia mtu upasuaji, akaendesha gari, akapika, n.k. Wakili roboti (DoNotPay) iliyotengenezwa na Joshua Browder. Aliivutiwa kubuni mfumo huo wa kisheria wa ushauri kwa wahamiaji kwa sababu bibi yake alikuwa mkimbizi kutoka Austria wakati wa vita vya Holocaust.


Jinsi roboti ‘DoNotPay’ anavyofanya kazi.

Roboti hiyo hufanya kazi kwa kuuliza msururu wa maswali kubaini kama mkimbizi anapaswa kulindwa na sheria za kimataifa. Inapofahamu kwamba mtumiaji anaweza kuomba uhamiaji, huchukua mamia ya maelezo na kutoa ushauri moja kwa moja kuhusiana maombi ya uhamiaji.


Chatbot-programu inayotumiwa na roboti kutoa ushauri kwa wahamiaji.
Lengo la kuundwa kwa ‘Wakili roboti’.

Awali iliundwa kwa ajili ya kuwasaidia watu kuondoka kwenye maeneo ya kuegesha magari ama kupata tiketi za mwendo kasi. Nchini Marekani na Canada, inawasaidia wakimbizi kukamilisha maombi yao ya uhamiaji, na nchini Uingereza, inaweza kuwasaidia wanaoomba uhamiaji kuweza kupata usaidizi wa kifedha kutoka kwa serikali.

Ni chatbot-programu ya kompyuta inayofanya mazungumzo kwa njia ya ujumbe na maagizo ya sauti na inatumia ujumbe wa Facebook wa Messenger kukusanya taarifa juu ya jambo na kutoa ushauri pamoja na nyaraka za kisheria.

Je, ina umuhimu?

Ndio, tena ina umuhimu mkubwa sana kutokana na kwamba maswali yote ambayo roboti hiyo huuliza ni ya Kiingereza kinachoeleweka na akili yake bandia hutengeneza majibu ambayo huonekana wakati wa mazungumzo.

Wakili roboti hupendekeza majibu ambayo mtumiaji anaweza kuyachagua ili kupunguza uwezekana wa maombi yake kukubaliwa.

Post a Comment

 
Top