Viongozi wa wa Ligi ya Premier Chelsea walipiga hatua kubwa kuelekea
kushinda ligi baada ya kuwanyuka Everton mabao matatu kwa nunge.
Mabao yote ya Chelsea yalifungwa katika kipindi cha pili.
Ina maana kuwa hata kama Chelsea itashuka kwa pointi tatu kwenye mechi
nne zilozosalia bado itachukua nafasi ya pili kwa miaka mitatu
mfululizia hata kama Tottenham watashinda mechi zote zilizosalia.
Iliwalazimu Chelsea kusubiri kabla ya kombora ya Petro lililotumbukia wavuni mnamo dakika ya 66.
Everton walikuwa wameanza kwa kasi kwa mwendo wa kazi ambapo Dominic Lewin nusura afunge.
Sare ya Manchester City na Middlesbrough ina maana kuwaa klabu yake
Ronald Koeman iko nyuma kwa pointi nane kutoka kwa klabu nne za kwanza
huku ikibaki na mechi tatu tu.
Post a Comment