Baada ya nusu fainali hiyo ya kwanza kupigwa leo itakuwa zamu ya Celta Vigo watakapoikaribisha Manchester United, kutoka katika jiji la Manchester ambalo United wapo hadi katika uwanja wa Celta Vigo nchini Hispania ni kilomita 1350, United wameshafika Hispania ambapo usiku wa leo watakabiliana na mtihani mkubwa dhidi ya wenyeji zao hao.
Manchester United rekodi yao dhidi ya timu za Hispania sio nzuri kwani United wamekutana na timu kutoka La Liga mara 47 ambapo katika mechi hizo United walishinda michezo 12, walifungwa 16, wakasuluhu michezo 19.
Lakini kwa upande mwingine mashetani hao wekundu katika nusu fainali zao 3 ambazo wameshawahi kucheza na timu za kutoka La Liga wameshinda nusu fainali mbili na kupoteza nusu fainali moja tu, na ikumbukwe Celta Vigo walifika hatua hii baada ya kuitoa timu ya Fc Genk anayochezea Mtazania Mbwana Samata.
Lakini usidhani ni rahisi hata kidogo kwa Manchester United kwani wapinzani wao wanaonekana wagumu sana msimu huu, katika michezo mitano iliyopita Celta Vigo hawajapoteza hata mchezo mmoja bali wameshinda minne na kusuluhu mchezo mmoja.
Manchester United ambao kocha wao ameshakutana na Celta Vigo mara 3 huku akiwafunga mara 2 na kupoteza mara 1 hadi sasa hawajapoteza hata mchezo mmoja katika michezo yao nane iliyopita katika mashindano hayo ya Europa
Habari njema zaidi kwa mashabiki wa Manchester United ni kwamba Eric Bailly na Paul Pogba wanaweza kuanza leo lakini pia Juan Mata yuko fiti kuwakabili Celta Vigo huku pia walinzi wao wawili Phill Jones na Cris Smalling wameonekana wakifanya mazoezi na timu.
Post a Comment