Hali
ya mtikisiko wa uchumi uliozikumba taasisi nyingi, hasa za fedha sasa
unazinyemelea benki tatu ambazo zinaweza kuwekwa chini ya uangalizi
maalumu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kama ilivyokuwa kwa Twiga
Bancorp.
Twiga
Bancorp, ambayo kwa sehemu kubwa inamilikiwa na Serikali, imewekwa
chini ya uangalizi wa BoT baada ya madeni yasiyolipwa (NPL) kuzidi
kiwango kinachotakiwa kisheria.
Hali
hiyo inazinyemelea taasisi nyingine tatu za fedh; Benki ya Wanawake
(TWB), ambayo pia inamilikiwa na Serikali, Ecobank Tanzania na Efatha
Bank, ambayo inahusishwa na taasisi ya kidini ya Efatha, kwa mujibu wa
uchambuzi wa The Citizen
Benki
hizo tatu zimelimbikiza kiwango cha NPL kinachozidi asilimia 50 ya
jumla ya mikopo iliyotolewa, huku kiwango cha Efatha kikifikia asilimia
63.
Wataalamu
wa benki wanaamini kuwa kiwango cha NPL kinachozidi asilimia 15 ya
jumla ya mikopo yote ya beki za biashara, kinaashiria uwezekano wa
kuanguka.
Katika
toleo la tisa la Hali ya Kiuchumi Tanzania, Benki ya Dunia
ilitahadharisha kuhusu kukua kupita kiasi kwa kiwango cha NPL, ambacho
kilifikia asilimia 9.5 mwaka 2016 kutoka asilimia 6.4 mwaka 2015.
Ripoti hiyo iliitaja TIB Development Bank ambayo kiwango chake cha NPL kilikuwa asilimia 38 katika robo ya kwanza ya mwaka 2017.
Hata
hivyo, taarifa za fedha za benki za biashara za robo ya kwanza mwaka
2017 zinaonyesha hali ni mbaya zaidi kwa Efatha, TWB na Ecobank
Tanzania.
Post a Comment