Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe
30 Aprili 2017, ameungana na waumini wa dini ya Kikristo kusali ibada
ya Jumapili katika Kanisa la Kiaskofu, Jimbo Katoliki la Moshi ,Parokia
ya Kristo Mfalme na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
Usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini mkoani Kilimanjaro na
kuwataka waumini wa makanisa hayo na Watanzania kwa ujumla kuendeleza
amani iliyopo nchini kwa kuwa ndio chachu ya Maendeleo.
Rais
Magufuli amesema hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya Tano
zina lengo la kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli ya taifa
linalomuamini MUNGU.
''
Napenda muniamini kuwa mimi nipo kwa niaba yenu, najua huu Urais si
wangu, Urais mnao ninyi mlioamuwa nitumike kama mtumishi kwa wakati huu,
nawaomba sana muendelee kuniweka katika sala zenu ili kazi hii ya Urais
isinipe kiburi, nikawe mtumishi wa watu'' Amesema Rais Magufuli.
Rais
Magufuli amewashukuru waumini wa makanisa hayo mawili na watanzania kwa
ujumla kwa kusimama pamoja kuliombea Taifa amani iliyowezesha wananchi
kupiga kura kwa amani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kutokana na
sala zao Mwenyezi MUNGU akamuwezesha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Aidha,
Rais Magufuli ametoa msaada wa mifuko 100 ya Saruji kusaidia maendeleo
ya kanisa Katoliki na Shilingi Milioni Moja kwa Kwaya ya Kanisa hilo ili
irekodi nyimbo zake, halikadhalka katika Kanisa la KKKT, Mheshimiwa
Rais ametoa mifuko 150 ya Saruji kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya
Kanisa hilo na Shilingi milioni Moja kwa Kwaya ya Kanisa hilo.
Nae
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama amemuunga mkono Rais Magufuli kwa
Kuchangia Mifuko hamsini ya Saruji ambapo Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro
Mhe. Said Meck Sadick amechangia mifuko hamsini ya Saruji na Shilingi
laki Tano.
Kwa
upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi ,Parokia ya Kristo Mfalme
Askofu Isaac Amani amemshukuru Rais Magufuli kwa uwamuzi wa kusali
kanisani hapo na kuwataka waumini wa kanisa hilo na Tanzania kwa ujumla
kuendelea kumuombea yeye pamoja na Serikali yake ili iweze kuwatumikia
Watanzania katika kuwaletea maendeleo na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya
mfano kwa Bara la Afrika.
Kwa
upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania -
KKKT, Askofu Dr Fredrick Shoo amewataka waamini wa kanisa hilo na
watanzania kwa ujumla kutokuwa na hofu kwa mambo yanayofanywa na Rais
hususani katika kupambana na maovu, dhuluma na ufisadi vikiwemo na
badala yake Watanzania wabadilike na kujijengea mazoea ya kufanya kazi
halali na kuwa waaminifu na kuwa wazalendo kwa Taifa lao.
Aidha,
Askofu Shoo amemuomba Dkt Magufuli kuangalia uwezekano wa kupunguza
kodi hususani kwa taasisi za kidini zinzotoa huduma za kijamii zikiwemo
zile za Elimu na Afya.
Akijibu
Maombi hayo Rais Dkt Magufuli amewaeleza waamini na watanzania kwa
ujumla kuwa Serikali inathamini michango ya huduma za kijamii
zinazotolewa na Taasisi za dini na kuahidi kuliangalia suala hilo.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU.
Moshi, Kilimanjaro.
30 Aprili, 2017.
Post a Comment