Shilole amebainisha hayo kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa Facebook ya EATV, Shilole baada ya kuulizwa swali na shabiki alidai kuwa yeye anapenda sana kutulia ila wanaume ambao huwa anawapata ndiyo huwa hawatulii jambo ambalo linamfanya yeye aonekane hajatulia.
"Sisi wanawake inapotokea upo katika mahusiano halafu ukaachana na mtu huyo unaonekana 'malaya' lakini kumbe siyo kweli wakati mwingine mtu unakuwa unashindwa kuvumilia matatizo ya mahusiano ukaamua kutoka kwenda kwa mwingine kwa kuwa siyo ndoa sasa ya nini niendelee kuteseka katika mahusiano". Alisema Shilole
Mbali na hilo Shilole amesema kuwa amekuwa na bahati mbaya sana kwenye mahusiano kwani mara nyingi kila mwanaume anayempata huwa yeye amewazidi umri jambo ambalo linafanya watu wahisi kuwa wanapenda kutoka na watoto wadogo.
"Kiukweli saizi siwakubali hao Serengeti boys, ila nina bahati mbaya maana kila mwanaume ambaye huwa ninampata unakuta nimemzidi umri kidogo, lakini kweli sipendi hicho kitu, mimi nampenda mwanaume yoyote yule ili tu anatakiwa awe anafanya kazi, hata kama ni mchota maji, mwanaume ambaye hana kazi sina muda naye kwa sasa maana hatakuwa na thamani ya kuwa mwanaume atakuwa ni 'Marioo' na mimi hao watu saizi hawana nafasi kwangu" alisisitiza Shilole
Post a Comment