0
Kiungo wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Himid Mao amewasili salama makao makuu wa klabu ya Randers inayoshiriki Ligi Kuu Denmark.

Himid ametua kwenye klabu hiyo kwa ajili ya kufanya maribio, na kama atafanikiwa kufuzu mtihani huo huenda akaihama Azam FC wakati wa usajili wa majira ya kiangazi.
Kama anavyoonekana  kwenye picha, akiwa katika uwanja anders  unaoitwa ‘BioNutria Park Randers’.

Kwa mujibu wa tovuti ya timu hiyo, inaeleza kuwa Himid atafanya mazoezi na kikosi kingine cha vipaji cha Randers leo Jumatano kabla ya Ijumaa kujumuika na timu ya wakubwa ya Randers.

Taarifa hiyo ya Randers inasema kuwa, Himid mbali na kufanya mazoezi atakuwa ni sehemu ya kikosi cha wachezaji wa akiba wa Randers kitakachocheza dhidi ya AC Horsens Jumanne ijayo kwenye Ligi ya Wachezaji wa Akiba ya nchini humo.

Post a Comment

 
Top