Vidonda vya tumbo ni ugonjwa unaotokea kutokana ukuta wa tumbo au utumbo mwembamba kutengeneza kidonda/vidonda.
Ukuta wa tumbo huwa unatoa gastriki yenye mchanganyiko wa asidi ya
haidrokloriki na vimenyenyo. Unapopata hamu ya kula au wakati unakula
asidi hii huzalishwa na tumbo ili kumenyenya chakula. Ukuta wa tumbo
hufunikwa na layer ya mucus ambayo huzuia asidi hii isitoboe ukuta wa
tumbo au utumbo mdogo.
Vidonda hivyo vya kwenye utumbo huweza kutokana na kutokula kwa wakati,
maambukizi ya Helictobacter pylori, kuvuta sigara au matumizi holela ya
madawa za kutuliza maumivu. asidi huzalishwa zaidi na hivyo kukwangua
ukuta wa tumbo au utumbo mwembamba na vidonda kutokea.
Jinsi ya kuishi na vidonda vya tumbo.
Acha kutumia kahawa na chai, kwa maana vitu hivi huongeza kiwango cha
asidi kinachotengenezwa na tumbo lako. Unaweza tumia chai ya mitishamba
Mfano mchaichai
Kula walau kidogo mara kwa mara. Hii itasaidia kupunguza athari za asidi inayotengenezwa na tumbo.
Epuka matumizi ya vileo kwani unywaji wa pombe mara kwa mara huweza kutonesha kwenye vidonda vya tumbo vinavyotaka kupona.
Epuka matumizi ya viungo vya vyakula kwa maana hufanya hali kuwa mbaya zaidi.
Kama ni mvutaji wa sigara basi acha kuvuta sigara/tumbaku/bangi. Uvutaji
wa sigara utakuweka kwenye hatari zaidi ya kuanza vidonda vipya na
kuzuia vidonda vingine visipone.
Post a Comment