Arsenal chali, klabu ya Arsenal leo walikuwa uwanjani zidi ya Sevilla na wakakubali kipigo cha bao 2 kwa 1 huku mabao ya Sevilla yakiwekwa kimiani na Joaquin Correa na Steven Nzonzi huku lile la Gunners likifungwa na Alexandre Lacazette.
Manchester United kwa upande wao wameendelea kufaidi matunda ya Lukaku kwani alifunga moja ya bao kati ya 3 walizowafunga Valerenga Fc huku mengine yakifungwa na Marouane Fellaini na Scott Mconimitay.
Pambano la mwisho kubwa lilipigwa usiku wa saa 6 ambapo As Roma walipambana na Juventus katika mpambano ambao uliamuliwa kwa matuta baada ya dakika 90 za mwanzo kuisha kwa sare ya moja kwa moja.
Katika hatua ya matuta klabu ya Juventus waliibuka kidedea kwa kupati penati zote tano huku As Roma wakikosa mkwaju mmoja wa penati hizo.
Valencia waliifunga 1 kwa 0 Afc Bournamouth, Lazio nao wakaifunga Bayern Leverkusen kwa mabao 3 kwa 1, huku Lyon na Montpellier zikienda sare ya bao moja kwa moja.
Post a Comment