Mshindi wa medali ya shaba katika mashindano ya riadha ya IAAF World Championship 2017 Alphonce Felix Simbu amerejea nchini pamoja na timu nzima na kupokelewa na watanzania wakiongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
Simbu alifanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya Tamirat Tola (Ethiopia) aliyemaliza nafasi ya pili na Geoffrey Kirui (Kenya) aliyeibuka mshindi wa mashindano hayo kwa upande wa wanaume.
Post a Comment