0
Image result for ozil eyes
Arsenal wamefanikiwa kumbakisha Mesut Ozil katika klabu yao, pamoja na tetesi nyingi zilizokuwa zikisemwa lakini Mesut anabaki na Arsenal kwa msimu mwingine wa mwaka 2017/2018.
Wakati dirisha la usajili likiendelea mengi yalisemwa kuhusu Ozil na wengine wakadai ni mpenda pesa anaweza kuondoka Arsenal, pamoja na yote hayo lakini Ozil hakuwahi kuongea lolote na alikuwa mkimya.
Hii leo baada ya ukimya wa muda mrefu Ozil afunguka kupitia Instagramna tena amefunguka haswa baada ya kutoa kile ambacho anaonekana alikuwa amekihafadhi moyoni kuhusina na mambo yanayoendelea Arsenal.
Chanzo cha ujumbe mzito wa Ozil anasema ni kutokana na maneno ya watu kuhusu Arsenal na vile vile maswali ambayo amekuwa akiulizwa na wachezaji wenzake kuhusu maisha ndani ya klabu hiyo.
Ozil ambaye anatimiza miaka minne tangia ajiunge na Arsenal anasema pamoja na kuhangaika mwanzo wakati anakuja ila ukubwa na historia ya Arsenal ilimvutia sana kujiunga na klabu hiyo ya London.
“Nilipokuja nilipewa nafasi nicheze kama winga wa kushoto, nilipata tabu kwakuwa sikuwa naifurahia nafasi hiyo, ninataka kucheza katikati na kuumiliki mchezo na kutengeneza nafasi” alisema Ozil.
Ozil anasema pamoja na ugumu wa ligi ya Uingereza lakini wamefanikiwa kubeba vikombe 6 tofauti ndani ya miaka minne na hilo sio jambo dogo japo hawajisikii vizuri kutokuwepo katika mbio za ubingwa wa Uingereza.
“Nakubali mimi ni ghali na nakubali nimemnunuliwa kwa pesa nyingi, watu wanatoa maoni wakiwemo wachezaji wa zamani waliofanikiwa na wasiofanikiwa katika klabi, mimi naona waache kuongea badala yake watuunge mkono” alisema Ozil.
Ozil amesema anashukuru kuwa mchezaji wa Arsenal na ana furaha kubwa kuvaa jezi ya washika mitutu hao wa London na kuwahakikishia ya kwamba yuko tayari kupambana kwa ajili yao.
Ujumbe wa Ozil unakuja siku chache baada ya Arsenal kufungwa bao 4 kwa nunge na Liverpool huku wachezaji wa zamani wa Arsenal akiwemo Martin Keown na Thiery Henry wakiwashambulia wachezaji wa klabu hiyo.

Post a Comment

 
Top