Katika habari ambayo imegonga sana vichwa vya habari wiki hii baasi ni mvutano kati ya msgambuliaji ghali duniani Neymar Dos Santos na mshambuliaji wa PSG Edison Cavanni.
Wafalme hawa wawili wameonekana kuvutana sana kuhusu nani atakayekuwa anapiga mipira ya adhabu karibu na lango la wapinzani na nani atakuwa akipiga penati.
Edson Cavanni amekuwa mpiga penati wa PSG kwa muda mrefu sana lakini Neymar pia ameonekana na ujuzi wa penati na hata akiwa Barcelona alikuwa akipiga baadhi ya penati.
Hali hii kati ya hawa wawili imeleta mvurugano ndani ya klabu ya PSG kiasi cha kupelekea wawili hawa kugombana katika siku za usoni wakigombea mipira ya penati.
Kocha wa PSG Unai Emery amesema kunahitajika hatua kufanya makubaliano katika sula la kupiga mipira ya penati na free kick katika michezo inayofuatia ya PSG.
Lakini Emery alipoulizwa kuhusu nani haswa ndio mpiga penati wao, alimalizia kwa kujibu hivi “mtu wa kwanza anayetakiwa kupiga penati katika timu yetu ni Cavanni na Neymar ndio anafuatia”
Post a Comment