0
Siasa zinazoendelea nchini Kenya huenda zikapelekea nchi hiyo kunyang’anywa uenyeji wa michuano ya CHAN inayotarajiwa kufanyika mwaka 2018 katika nchi hiyo.
CAF kupitia kwa makamu wa rais wa pili Costantin Omary walikuwa wakitarajiwa kufika Kenya September 3, 2018 kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa viwanja na masuala mengine(usalama, miundombinu, malazi, n.k)  ambayo yanahusu uandaaji wa michuano ya CHAN.
Kutokana na hali ya kisiasa na masuala ya uchaguzi nchini Kenya kuna dalili za CHAN kuhamishwa kutoka Kenya kwenye katika nchi nyingine, Morocco na Afrika Kusini ni mataifa ambayo yanatajwa huenda yakapokea kuandaa michuano ya CHAN 2018.
Uchaguzi wa Kenya ambao utakuwa ukirudiwa huenda ukafanyika ndani ya siku 60, ukianga sasa hivi ni mwezi September kwa hiyo siku 60 baadaye itakuwa ni mwezi November na lolote linaweza kutokea hapo katikati. CAF wameamua kuchukua hatua za dharura kabla mambo hayajawa mabaya.
Vicent Otien ni mwandishi wa habari kutoka kituo cha Nation amesema ukiachilia mbali masuala ya kisiasa nchini Kenya, bado nchi hiyo haitakuwa tayari kuandaa michuano ya CHAN kutokana na viwanja kutokuwa tayari hadi sasa.
“Rais wa shirikisho la soka la Kenya Nick Mwendwa alitembelea uwanja wa Nyayo ambao ni miongoni mwa viwanja vitano vilivyoratibiwa kuchezewa michuano hii lakini baadae akatoa taarifa kwamba ile kamati ya ukaguzi kutoka CAF haitafika nchini na bada yake naibu Rais wa CAF Costant Omary atafika nchini kuangalia hali tete ya kisiasa ili kujua kama Kenya itakuwa tayari kuandaa michuano hiyo au vinginevyo.”
“Viwanja vinne havipo tayari hadi sasa, ni kiwanja cha Kasarani pekee ndiyo kipo tayari hadi sasa lakini uwanja wa Nyayo ndio wameanza kuukarabati, uwanja wa Kinoru  hawajamaliza sawa na uwanja wa Machakosi ambao ukarabati ndio umeanza. Mafundi wanasema itachukua muda wa wiki 14 kukamilika kwa ukarabati sawa na miezi miwili na nusu”
“Wataalam wengi wanasema Kenya haitokuwa tayari kuandaa michuano hiyo ukiachilia kwa hali ya viwanja ilivyo mbali masuala ya hali ya kisiasa ya Kenya.”
“Masuala ya siasa ya Kenya yanachangia kwa kiasi fulani ikiwa ni baada ya mahakama kuamuru uchaguzi wa Kenya kurudiwa ndani ya siku 60. Sasa hivi ni kampeni tu ndio zinaendelea watu hawafikirii kabisa shughuli za kimpira.”

Post a Comment

 
Top