Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ametoa agizo hilo leo Alhamisi.
Halmashauri hizo ni Mwanza, Mbeya, Moshi, Singida, Kigoma, Karatu, Mbinga, Pangani, Mbinga, Morogoro, Igunga na Kongwa.
Jafo amesema hadi Septemba 30 bodi imetoa mikopo yenye thamani ya Sh9.7 bilioni kwa halmashauri 54 nchini.
Amesema hadi Septemba 30 fedha zilizorejeshwa ni Sh6.6 bilioni.
"Halmashauri nyingi zimejitahidi kurejesha mikopo kwa wakati lakini kuna zilizoonyesha usugu katika kurejesha mikopo," amesema.
Amesema kutorejeshwa kwa mikopo kunasababisha halmashauri nyingine kukosa fursa ya kukopa.
Jafo ameiagiza bodi kuangalia utaratibu wa kupitisha mikopo inayolenga ujenzi wa viwanda na uwekezaji katika halmashauri ili kukuza ajira na uchumi wa viwanda.
"Bodi iache kubweteka, ijipange kimkakati kujenga uwezo mkubwa wa kutoa mikopo kwa halmashauri zilizo makini katika mapinduzi ya viwanda," amesema.
Post a Comment