Akiongea na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Lady Jaydee amesema ni jambo jema na la kumshukuru Mungu kwa wasanii wanapopeana ushirikiano.
“Ni jambo jema msanii mwenzako anapokusuport, na ndio kitu ambacho wasanii wengi tunapenda, sisi binadamu kwa hivyo mkae mkifahamu kwamba hakuna marefu yasiyo na ncha, nilishukuru kwamba msanii mwenzangu amenisuport”, amesema LadyJaydee.
LadyJaydee ameendelea kwa kusema kwamba.... “ni wasanii ambao tulikuwa tunaelewana, na ndio maana tuliweza kufanya nyimbo nyingi ambazo ziliweza kufanya vizuri, watu walikuwa wanasikitika kwa yale yaliyotokea”.
Wawili hao walikuwa kwenye bifu kali ambalo ilikuwa hata salamu hakuna, lakini hivi karibuni wameamua kuyamaliza na kuondoa tofauti zao.
Post a Comment