Habari kubwa sana mwishoni mwa wiki iliyopita na mwanzo mwa wiki hii ni suala la upigaji kura kwa raia wa Catalunya ambao ulitakiwa kufanyika jana lakini polisi wakavamia wqpiga kura.
Gerrard Pique ni kati ya wachezaji ambao mara nyingi wamekuwa wakionesha hisia zao kuhusu mapenzi yao na Catalunya, Pique ameweka wazi kwamba ameumia sana kutoka na kile kilichotokea siku ya jana.
Pique aliyekuwa akitokwa na machozi amesema polisi wa Hispania wamewafanyia ndugu zake kitendo kilichomuuma sana na ni tukio baya kuwahi kumtesa tangu aaanze maisha yake ya soka.
Pique ameeleza wazi kwamba yeye hakuwa anatamani mchezo wao na Las Palmas uwepo lakini Palmas walilazimisha mchezo uwepo na kwa kushirikiana na chama cha soka cha Hispania walifanikisha tukio hilo.
Pique anasema babu na bibi yake pamoja na watoto wao walitamani sana tukio la kupiga kura kuikomboa Catalunya lakini jambo la ajabu polisi waliwapiga na kuwaumiza bila sababu maalum.
“Nilijua polisi watajaribu kuzuia upigaji wa kura lakini niliamini watatumia njia ya amani kujaribu kuzuia hilo, walichofanya jana kimeleta daraja kubwa kati ya Catalunya na Hispania huku chuki inaweza ongezeka” alisema Pique.
Pique anasema kilichomuumiza zaidi ni baada ya kuona picha na video zinazosambaa mitandaoni za polisi wakitumia nguvu kubwa kuwashambulia raia ambapo watu zaidi ya 406 waliumia.
Pique aliulizwa ni nini atafanya kuhusu timu ya taifa ya Hispania? “Nitaendelea kuitumikia lakini kuna watu wananiona mimi ni tatizo, kama mimi ni tatizo naweza nikasogea pembeni”
Kuhusu mchezo dhidi ya Las Palmas Pique amesema “nilitamani mchezo uishe tangu unaanza na kila saa niliangalia mda unavyokwenda, sikuwa na furaha”
Post a Comment